JICHO NDANI YA QATAR


 Hawa Ecuador walitoa sare na wababe wa South America , hawa ndio wamefuzu mbele ya Chile ya kina Vidal na Sanchèz.... kiukweli Qatar walikuwa hawana namna nyingine kwa jinsi Ecuador walivyokuwa wanacheza "Total Dominace".


Nini kingine Qatar wangefanya zaidi ya hapo? , walikutana na Ecuador ambayo ilikuwa bora kila eneo la uwanja maji marefu kwa Qatar.... Ecuador walikuwa na Back 3 wakati wanashambulia (Wa 3 nyuma then Caicedo anakuwa mbele yao kutengeneza pembe tatu , alafu mawingback wanatanua uwanja zaidi kufungua njia za kupokea mipira , ilikuwa rahisi kwao kutokaka na Qatar wakati wanaenda kupress walikuwa na wachezaji wawili eneo la mbele ngumu kutokana Ecuador wanawa out numbers Qatar ilikuwa 2 vs 4 .... Back 3 + DM rahisi kwa Ecuador kusogea juu.

.

Ecuador wakati wanaenda kushambulia walipata nafasi kubwa kwenye nusu ya mpinzani , kutokana na Qatar kutoweka presha kwenye mpira na kwa mpinzani , kitu ambacho kiliwafanya Ecuador wapate space kubwa pembeni mwa uwanja na kwa mshambuliaji wao kiongozi.... Qatar wasipokuwa na mpira wanakuwa kwenye shape ya 5-3-2 lakini bado walishindwa kuweka ukuta ambao ungekuwa mgumu kupitika.

.

Second Half , Qatar waliamua kuzuia tu , tofauti na kipindi cha kwanza ambao walikuwa wanazuia kuanzia juu na watu wawili , walilenga kutengeneza mashambulizi kwa kushtukiza lakini Ecuador walikuwa wagumu kufunguka.

.

✍🏻 Enner Valencia ndio Jina ambalo litaimbwa leo pale Qatar👏 Jamaa katili sana mbele ya lango🔥

.

✍🏻 Moises Caicedo mwamba anaubonda sana 🙌 DM yake haina mambo mengi (Ni Passer mzuri  anafanya Blocking na rahisi sana kunusa hatari.... nadhani ni almasi ndani ya kikosi cha Ecuador)

.

✍🏻 Labda mnitajie mchezaji wa Qatar ambaye anaweza kuwa Man of The Match kwa upande wao😀 Who?

.

✍🏻 TUMEENJOY MECHI YA KWANZA IKIWA NA MAGOLI👏


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JIFUNZE NAMNA YA KUPIKA TAMBI