MBARONI KWA KUMUUA DEREVA TAKSI NA MWANAFUNZI
0 0 Ramadhani Ng’anzi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Jeshi la Polisi jijini Mwanza linawashikilia watu tisa kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Nicholus Telesphory (25) na dereva taksi, Respikius Anastaz (55). Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng’anzi amesema watu hao walikamatwa maeneo tofauti mkoani humo. Ng’anzi amesema Januari 29, 2022 katika mtaa wa Ng’washi kata ya Buhongwa wilayani Nyamagana mwanafunzi wa SAUT aliyekuwa akisoma shahada ya kwanza ya Uhusiano wa Umma na Masoko, Nicolaus Telesphory aliuawa kwa kushambuliwa na kundi la watu wakimtuhumu kuiba televisheni. Amesema kwa sasa wanaoshikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi huyo ni watu watano “Marehemu alifariki akiwa katika hospitali ya rufaa ya Kanda ya Bugando alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa kutumia mawe na fimbo kwenye maeneo mbalimbali ya mwili wake,” amesema Ng’anzi Katika tukio lingine Kamanda Ng...